Insha
Za Karne

By

Henry Wao

Copyright © 2014


All rights reserved by Henry Wao
No part of this book may be reproduced or transmitted in any form or by any means,graphic,electronic,or mechanical including photocopying,recording,taping orby any information retrieval system, without permission in writing of the publisher.
Ariba Technologies & Book Publishers
P.o Box 503-40600
Siaya –Kenya
Website: www.aribatecbp.com
E mail: admin@aribatecbp.com
Cell: +254 723 987926

ISBN:  978-1495951251

 

First published 2014

YALIYOMO
 

SHUKURANI……………………………….

DHAMIRA
4
1 TUZO KWA ABU…………………….……. 6
2 INSHA……………………………….……… 8
3 SARUFI………………………………….…. 10
4 KIUNGANISHI “NA”…………………….. 12
5 TAMATHALI ZA LUGHA …….…….….. 13
6 ISHARA ZA WANADAMU…...….............. 21
7 VINYUME……………………..…...………. 29
8 METHALI…………………..……................ 36
9 TASHBIHI…………………..…………....... 38
10 TANAKALI…………………..……………. 41
11

TASHDIDI……………………..…………...

42
12 MISEMO……………………..…………….. 43
13 UAINISHAJI WA MANENO KATIKA SENTENSI 49
14 AINA ZA INSHA………………….............. 53
15 MWONGOZO WA KUTAHINI……….. 92

SHUKURANI.

Nitakuwa mchache wa fadhila nisiposhukuru shirika lililo chapisha kazi hii adhimu na vilevile kuwatambua wafuatao waliochangia kwa njia moja au nyingine kunipa shime, motisha na morali kualifu kitabu hiki.Moses Okello ambaye ni mjuzi wa ngamizi.
Ustadh wallah bin wallah, mwadhamu Ken Walibora, washikadau wote katika kipindi cha bahari ya lugha. Mheshimiwa Charles Obiero wa Liganwa. George Agan, Daniel Odhiambo wote wa Liganwa, Maselus Ochieng, Omiena Steve na sahibu yangu Alphonce Odero wote tuliofanya nao bega kwa bega kuinua kiwango cha lugha kule Ng’ura.Bwana Joannes Opondo wa Dibuoro.
Sitawasahau mheshimiwa Levy Amwai aliyekuwa Bishop Okoth Mbaga, Shikanda, Denge, na wote tuliokongamana nao katika hafla, warsha na usahihishaji wa mtihani wa wanafunzi wa kidato cha nne kule Ng’iya.Elisha Otieno kwa kunaksisha jalada.Peter Akello wa Unna.
Walimu wote tuliofunza nao katika shule ya St. Julian’s Academy. Mheshimiwa Linus Ogutu. ambaye ni mwalimu mkuu wa Nyambare na Jack Stephen Obola mswahili wa kupigiwa mfano. Clement Abungu wa Nyandheho, Mbinga, Daniel na Steve wa Sidok.Mheshimiwa George Ogutu na Ustadh Francis wa Sidundo.Bwana Adwera Mhongo na Julius Ogalo.
Mheshimiwa Enock Oreda, Simon Ogutu, David Obwaka,Erick Olwanda, Victor Okochi, Raphale Oduol, AndrewOngoli,Serfin,Judith,Winney,Monica,Nelly,Josephine na wachapa kazi wote wa Uwasi waliopeperusha bendera ya shule na kuiletea sifa tolatola.Bwana Francis Musewe,Thomas Otieno na Nelson Juma ambao ni wa wakilishi katika chama cha walimu KNUT.
Peter Akelo wa Unna, Joseph Kibwana, Patrick Omondi na Ponsianus Ochieng wa Barding. Mwisho zaidi ni kwa walimu wote tuliokuwa nao katika chuo cha walimu Moi, Baringo. Fredrick Akelo wa Siaya Township na Nyagaya Komolo.Mwadhamu Dalmas Owuor-Kasisi Muhtasi wa Gilgom-Nyadorera.

Ndugu zangu Helen Malowa, Andrew Malowa wa Wilson,Grace Agola, Julia Wao, Eunice Wao, William, Dan, Charles, Mark na dadangu mpendwa Mary Amondi Wao wa chuo kikuu cha Masinde Muliro,mahasibu na mahasidi wote siwezi kuwataja bali nawapa pongezi sufufu kwani bila nyinyi nisingefika nilipo.Maulana awajalie mema kwa kuwapa baraka za kazole ili mzidi kukiendeleza na kukisanifisha Kiswahili.Rabbi Alamina ndiye alfa na omega.
  1. DHAMIRA

Kitabu hiki kimetungwa kutokana  na utafiti kidinya wa hapo awali kuhusu vipengele mbalimbali vya lugha. Ni kitabu cha pekee tangu enzi za akina Hayati Shaban Robert kukusanya misamiati mipana ya magonjwa, michezo, samaki, mapambo ambayo haipatikani katika kitabu chochote.
Kinazindua wasomi kuendelea kusoma,kuiheshimu lugha hii. Wanaojitayarisha kwa mtihani wa kitaifa (K.C.P.E) ,ngeli zimerahisishwa na mifano kadhaa ya maneno katika ngeli husika kuorodheshwa. Wanafunzi wa vidato vya kwanza hadi pili pia watanufaika. Mwelekeo mbaya wa kuandika aya mbili au tatu katika insha za barua umetupwa mbali na muundo halisi kuoneshwa.
Kitabu chenyewe kinamsaidia mwalimu na wanafunzi kuelewa mandhari yao yalivyo. Taksiri pamoja na tashtiti katika mazungumzo ya kawaidha au kupitia idhaa mbali mbali zimeondolewa na msomaji kutandikiwa tandiko laini tena jema.
Vipengele vyote vya uandishi vimeshughulikiwa kulingana na matakwa ya silabasi. Ubunifu, mtindo,tamathali za lugha ,msamiati mwafaka pamoja na mifano kadhaa ya insha aula.
Tumefanya utafiti wa kurekebisha yote.
Ubora wa kitabu hiki ni kukisoma na bila shaka utagundua kuwa umebadilika na kuwa mtu tofauti kinyume  cha jinsi ulivyokuwa awali.
Kiswahili aula, ujenzi wa taifa.
Pateni uhondo.

TUZO KWA ABU

Waama watangulizi, baba kichwa cha nyumba,
Batinini mwendo zazi, nina eti avya mimba,
Abu kwake nyendezi, kanivusha ule msimba,

Daraja nilivukalo, yamkini ni mlingoti,
Danguroni ni kololo, kaniacha maututi,
Dirhamu na liwalo, jinzi kasomba nyutiti.

Kortini ukapelekwa, kwa masa na masaibu,
Afisi za watoto kwa hoji zote ukajibu,
Mola tu ndiye sirikwa, kwa machungu ya ububu.

Wengi wasi babazo, makwao hayaendeki,
Baba haki mwongoza, utumwani hukaliki,               
Nasaha zako ninazo, kurunzi yangu tariki.

Wema wako washamiri, vijijini majijini,
Mama uzazi hiari, malezi ya mipipani,
Kwako ureda ni furi, mnofu fupi njiani.

Mkono kulea mwana, baba wazidi watano,
Kwa udi pamwe uvumba, nikawa ja msumeno,
Hayawani macho vimba, mbwakoko ni lingano.
Tamatini nifikapo, majonzi yanisakama,
Hata ndege duni japo, makinda huwapa hima,
Viokote mwaonapo, mama zao wa wazima.

Heri usiwape enzi, kuwadhulumu wanao,
Rehema funga zingizi, utunze uwapendao,
Kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana,

Waadhi.
Raghba niliyo nayo ilinipa msukumo kuandaa hiki kitabu ili niendeleze lugha fasaha katika bara letu.
Kuna upyoro, utohozi na kubandikwa kwa maneno mengi yasiyofaa katika matumizi ya lugha hii tukufu.
Katika utunzi wa mashairi tunamshairi, malenga na shaha. Watu si sawa kama vidole kwenye kitengele lakini tusipiganie ubingwa tukapotosha limbukeni.
Mabingwa wa uongo kama manabii wanao dai kuhotesha tasa wakakopoa pacha wamejaa mijini na mashambani. Waliotakadamu waliyanywa maji maenge lakini tukumbuke kuwa kutangulia sio kufika. Ndege akiwa hai hula wadudu lakini anapokufa mzoga wake huliwa na wadudu.
Mbaruti huweza kuunda njiti alfeni za vibiriti ilhali kibiriti huweza kuteketeza msitu mzima.
Lazima twende na wakati.

 

Nunua kwa Kshs 500 uendelee kusoma